Kama vile Mungu Alivyozamisha jeshi la Misri katika Bahari ya Shamu, Aliharibu nguvu ya dhambi na kuwapa wanadamu tumaini la ufufuo katika Siku ya Ufufuo.
Ni siku ambayo Yesu Mwenyewe Alituonyesha kwamba tutabadilishwa kutoka mwili wa asili kuwa na mwili wa kiroho.
Siku ambayo jeshi la Misri lilizikwa katika Bahari ya Shamu na Waisraeli walipovuka ng'ambo kutoka Bahari ya Shamu ilikuwa Jumapili.
Kwa hiyo, ili kuadhimisha siku hii, Siku ya Malimbuko katika Agano la Kale ilianzishwa na sikuzote iliadhimishwa siku ya Jumapili.
Kulingana na unabii huo, Yesu Kristo Alifanyika tunda la kwanza la wale waliolala naye Akafufuka kutoka kwa wafu siku ya Jumapili.
Lakini uenyeji wetu uko mbinguni. Nasi tunamngoja kwa shauku Mwokozi kutoka huko, yaani, Bwana Yesu Kristo,
atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, ili upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote chini yake.
Wafilipi 3:20–21
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha