Kupitia mfano tuliopewa na Yesu, tunapata kuelewa kwamba Abrahamu
anamwakilisha Mungu Baba, na kwamba Sara, ambaye alikuwa na jukumu
muhimu katika kuamua warithi wa familia ya Abrahamu, ni Mama yetu,
ambaye yuko huru na anawakilishwa kama agano jipya.
Wale wasiomwamini Mungu kabisa kama Eliezeri, ambaye wazazi
wake walikuwa watumwa, au wale wanaomwamini Mungu Baba tu,
kama Ishmaeli, hawawezi kuwa warithi wa Mungu.
Kama Isaki, wale wanaompokea Mungu Baba (Kristo Ahnsahnghong)
na Mungu Mama, ambao wako huru, na wametiwa muhuri kama, “Watoto
Wangu,” kwa njia ya mwili na damu ya Mungu, wanaweza kuwa warithi wa
ufalme wa mbinguni.
“Yule tajiri naye akafa na akazikwa.
Kule kuzimu alipokuwa akiteseka, alitazama juu,
akamwona Abrahamu kwa mbali, naye Lazaro alikuwa karibu yake.
Hivyo yule tajiri akamwita, ‘Baba Abrahamu, nihurumie . . .’ ”
Luka 16:22–24
Lakini, mtoto wa mwanamke mtumwa alizaliwa kwa mapenzi ya mwili, na
yule mwingine wa mwanamke huru alizaliwa kutokana na ahadi ya Mungu.
Mambo haya yanaweza kuchukuliwa kama mfano . . . ndugu zangu,
sisi si watoto wa mwanamke mtumwa, bali wa yule aliye huru.
Wagalatia 4:23–31
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha