Tunapoangalia nyuma kwenye maisha yetu, tunatambua kwamba tumepokea msaada kutoka kwa mshauri mara nyingi kufika hapa tulipo leo.
Huwezi kufanya kila kitu kikamilifu peke yako bila kupokea msaada kutoka kwa mtu mwingine.
Kwa maneno mengine, sehemu kubwa ya mafanikio yetu inategemea mshauri wetu ni nani.
Leo, Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu linaendelea kukua na kuushangaza ulimwengu.
Kanisa la Mungu limepokea tuzo nyingi za rais, kama vile Tuzo ya Malkia wa Uingereza kwa Huduma za Kujitolea, vyeti vitatu tofauti vya rais nchini Korea, na Tuzo ya Huduma ya Kujitolea kwa Marais wa Marekani.
Je, mshauri wa Kanisa la Mungu aliyelifanikisha hili ni nani?
“Watoto wako wote watafundishwa na BWANA, na amani ya watoto wako itakuwa nyingi.” (Isa 54:13)
Nabii Isaya alitabiri kwamba Mungu Atakuwa mshauri wetu.
Katika Isaya “watoto wako” humrejelea nani?
Tunaposoma mistari iliyotangulia, tunatambua kwamba “watoto wenu” wanawakilisha watoto wa mji wa
Yerusalemu.
Basi, Yerusalemu Anamrejelea nani?
Lakini Yerusalemu wa juu ni huru, nayo ndiye mama yetu. (Gal 4:26)
Uhalisi wa Yerusalemu ni Mama yetu wa Mbinguni.
Kwa hiyo, watoto Wake ni wale ambao watafanikiwa kweli kweli kuingia katika ufalme wa mbinguni.
Kanisa la Mungu ndilo kanisa pekee leo linalomwamini Mungu Mama.
Mama yetu wa Mbinguni, ambaye anakaa nasi leo, ndiye mshauri wa Kanisa la Mungu.
Kwa sababu hii, Kanisa la Mungu linafanikiwa katika kila kitu wanalofanya.
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha