Kama jina linavyodokeza, Pasaka ya agano jipya ni sikukuu ambayo kwa hiyo maafa hupita juu. Nguvu ya Pasaka ya agano jipya, ambayo inaruhusu maafa kupita juu, inabaki kuwa kweli hata leo.
Kwa bahati mbaya, watu wengi hawatafuti kupokea ahadi hii ya hakika. Bila shaka, kunaweza kuwa na sababu wanaiona kuwa vigumu kuamini, lakini kwa usahihi zaidi, ni kwa sababu wana uhakika usio dhahiri kwamba maafa kama hayo hayatawapata.
Ilikuwa vivyo hivyo katika wakati wa Nuhu. Hata wakati Nuhu alitumia miaka hiyo yote kujenga safina kubwa, na hata mvua ilipoanza kunyesha, watu wa wakati huo waliendelea na maisha yao ya kila siku bila wasiwasi. Hawakuona mbele kwamba mvua ingebadilika kuwa mafuriko.
Kwa njia hii, maafa hayatabiriki. Haiwezekani kujua kikamilifu lini, wapi, na aina gani ya maafa yatatokea na kujiandaa kwa ajili yao ipasavyo. Bila shaka, ni heri ikiwa tuna bahati ya kutosha kuokoka katikati ya maafa, lakini je, si ni hatari sana na uzembe sana kuachia kila wakati kwa bahati?
Wanadamu wote wanahitaji ahadi ya hakika ya Mungu. Ahadi hiyo ni Pasaka ya agano jipya, ambayo kwa hifyo maafa hupita juu.
00:00 Gharika ya Nuhu
00:51 Sababu Hawakuingia Safina
01:57 Hali ya Wale Walioachwa Nyuma
02:42 Maafa ya Leo
03:12 Tiba ya Maafa: Pasaka ya Agano Jipya
04:10 Si kuhusu Bahati au Nasibu, bali Ahadi ya Hakika ya Mungu
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha