Jehanamu ni mahali pa kutisha sana ambapo ni vigumu hata kupokea tone la maji ukiwa katika uchungu wa moto. (Luka 16:24) Yesu Alisema ikiwa mkono, mguu au jicho letu linatufanya tutende dhambi, ni afadhali kukata au kung’oa kuliko kwenda jehanamu. (Marko 9:43) Ni kwa sababu mateso ya jehanamu hayawezi kulinganishwa na maumivu ya kukatwa sehemu ya mwili wetu.
“Mahali ambako funza wake hawafi wala moto wake hauzimiki katika jehanamu.” Marko 9:48
“Kila mtu atatiwa chumvi kwa moto.” Marko 9:49
Ingawa adhabu ya jehanamu ni chungu sana, hatuwezi kufa kwa peke yetu. Kwenye jehanamu, hakuna wakati wa furaha ya maisha, hakuna wakati wa kupumzika, na hakuna tumaini la wokovu hata kidogo, lakini tu maumivu makubwa, majuto na huzuni. Kwa nini tunaenda jehanamu ikiwa hatutubu baada ya kusikia injili?
Kabla hatujazaliwa katika dunia hii, tulikuwa malaika mbinguni. (Ayubu 38:4-21) Hata hivyo, tulitenda dhambi mbinguni na tukapokea hukumu ya kwenda jehanamu. Kwa hivyo tulizaliwa duniani, gereza la kiroho, na tunakaa hapa kwa muda. (Ezekieli 28:13-17) Ikiwa hatutafuti njia ya kukwepa adhabu ya jehanamu hapa duniani,
“Ole wangu mimi maskini! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?” Warumi 7:24
Mungu Aliwahurumia wanadamu waliokusudiwa kupokea adhabu ya jehanamu, na Yeye Mwenyewe Alikuja hapa duniani ili kuonyesha njia ya kuepuka adhabu ya jehanamu.
“ . . . kuwaita . . . wenye dhambi wapate kutubu.” Luka 5:32
Ili kusamehe dhambi zetu zinazoongoza kwenye kifo na kutuokoa kutokana na adhabu ya jehanamu, Mungu Alitoa mwili na damu Yake kuwa fidia kwa ajili ya wanadamu, wenye dhambi.
“ ‘Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu.’ ” Mathayo 26:26
“ ‘Divai ya Pasaka ni damu yangu ya agano, inayomwagika kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.’ ” Mathayo 26:28
Tunapoadhimisha Pasaka ya agano jipya, tunabarikiwa na msamaha wa dhambi na kuokolewa kutokana na adhabu ya jehanamu. Na pia, tunaweza kupokea uzima wa milele na kurudi mbinguni.
“ ‘Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.’ ” Yohana 6:54
Hata hivyo, tukikataa ujumbe, “Pokea msamaha wa dhambi na uzima wa milele kwa njia ya Pasaka,” dhambi tulizofanya mbinguni haziwezi kusamehewa, na tunapaswa kupokea adhabu ya jehanamu kama ilivyokusudiwa.
“ ‘Nimetamani sana kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu.’ ” Luka 22:15
Tafadhali adhimisha Pasaka ya agano jipya, ishara ya Mungu ya msamaha wa dhambi, na urudi mbinguni!
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha