Abrahamu alitoa zaka kwa Melkizedeki aliyembariki kwa mkate na divai, na Daudi akatabiri kwamba “kuhani wa milele anayefuata kwa mfano wa Melkizedeki ni Mungu.” Pia, Mtume Paulo alishuhudia kuhusu Kristo ambaye Atakuja tena katika Enzi ya Roho Mtakatifu kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, kwa kueleza kwamba “Melkizedeki hana baba wala mama wala nasaba.”
Melkizedeki wa Agano la Kale alimpa Abrahamu baraka ya kimwili kupitia mkate na divai. Vivyo hivyo, Yesu Alitoa baraka ya msamaha wa dhambi na uzima wa milele kupitia mkate na divai ya Pasaka ya agano jipya. Kristo Ahnsahnghong Alishuhudia kwamba Yeye ni Mungu Aliyekuja kwa Mfano wa Melkizedeki, kwa kurudisha Pasaka ya agano jipya ambayo ilikuwa imebaki kuondolewa kwa miaka 1,600.
Baada ya Abramu kurudi kutoka kumshinda Kedorlaoma na wafalme walioungana naye, . . . Ndipo Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai. . . . Kisha Abramu akampa sehemu ya kumi ya vitu vyote. Mwanzo 14:17–20
Hivyo wanafunzi wakafanya kama vile Yesu alivyokuwa amewaelekeza, nao wakaandaa Pasaka. Yesu alichukua mkate, na baada ya kushukuru,. . . Kisha akatwaa kikombe [divai], na baada ya kushukuru, . . . Hii ndiyo damu yangu ya Agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi. Mathayo 26:19–28
Juu ya mlima huu Bwana Mwenyezi Ataandaa. . . karamu ya divai ya zamani . . . atameza mauti milele. Katika siku hiyo watasema, “Hakika huyu ndiye Mungu wetu; tulimwamini, naye akatuokoa.” Isaya 25:6–9
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha