Katika bustani ya Edeni, kulikuwa na Mti wa Ujuzi wa Mema na Mabaya, ambao Mungu Alisema,
“Siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa,” na Mti wa Uzima ulioleta uzima wa milele kwa
mtu yeyote aulaye. Walakini, Adamu na Eva walijaribiwa na nyoka na kutotii amri ya Mungu
kutokula lile tunda lililokatazwa. Matokeo yake, hawakuruhusiwa tena kula kutoka kwenye Mti wa
Uzima lakini wakaja kufa.
Uhalisi wa Mti wa Uzima ni Pasaka ya Agano Jipya ambayo kupitia hiyo tunakula mwili wa Yesu na
kunywa damu Yake. Ili kutuokoa kutoka dhambi ya kula lile tunda lililokatazwa– inayostahili kifo,
Mungu Ametupa nafasi moja zaidi ya kuiadhimisha Pasaka–kuiadhimisha katika mwezi wa pili
kulingana na kalenda takatifu.
Pasaka iliondolewa katika mwaka 325 BK, na njia ya kuuendea Mti wa Uzima ilikuwa imefungwa
tena. Kristo Ahnsahnghong, mwanzilishi wa Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu,
Amefungua njia tena, kulingana na unabii wa Biblia.
. . . karamu ya mvinyo wa zamani . . . atameza mauti milele . . .
Katika siku ile watasema, “Hakika huyu ndiye Mungu wetu . . .” Isaya 25:6–9
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha