Makanisa mengi sana ulimwenguni husisitiza kwamba
mafundisho yao yako sahihi. Miongoni mwa hayo, je, kanisa lipi
ndilo kanisa la kweli ambalo linaweza kurithi Ufalme wa Mbinguni?
Tunaweza kupata jibu katika historia ya familia ya
Abrahamu kwamba Kanisa la Mungu ndipo Anapokaa Mungu Mama.
Kulikuwa na wagombea watatu kwa ajili ya urithi
wa familia ya Abrahamu. Mgombea wa kwanza alikuwa ni Eliezeri, mtumishi;
mgombea wa pili alikuwa ni Ishmaeli; na mgombea wa tatu alikuwa ni Isaki.
Sababu Isaki aliye mdogo zaidi, na si Ishmaeli
mzaliwa wa kwanza wa kiume, aliweza kuwa mrithi wa Abrahamu
bila shaka ilikuwa kwa sababu ya mama yake Sara, yaani mwanamke huru.
Familia ya Abrahamu inawakilisha mfumo wa Mbinguni.
Ijapokuwa kuna makanisa mengi leo, ni kanisa tu linaloamini
katika Mungu Mama huyo mwanamke huru na
kumfuata Yeye, linaloweza kuwa mrithi wa Mungu kama Isaki.
Lakini Yerusalemu wa juu ni huru,
nayo ndiye mama yetu.
Wagalatia 4:26
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha