Katika Talmud, kuna hadithi kuhusu mwana ambaye anatambua siri iliyomo katika wosia wa baba yake na kurithi mali ya baba yake. Ili wanadamu waweze kurithi ufalme mtukufu wa mbinguni, ni lazima waelewe maneno ya Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama, ambayo yamo katika vitabu 66 vya Biblia.
Kuhani mkuu pekee ndiye angeweza kuingia Patakatifu pa Patakatifu, na siku moja tu katika mwaka. Siku hii ilikuwa Siku ya Upatanisho. Yesu Alipokufa, pazia la patakatifu lilipasuka na njia ya kwenda Patakatifu pa Patakatifu ikafunguliwa.
Kuanzia sasa na kuendelea, ni lazima wanadamu wapitishe dhambi ya kifo ambayo walitenda mbinguni kwa Shetani, ambaye anawakilishwa kama mbuzi wa kubebeshwa dhambi. Na ili kutekeleza upatanisho wa milele, lazima waje kwa Mungu Mama, ambaye ndiye uhalisi wa Patakatifu pa Patakatifu.
Yesu alipolia tena kwa sauti kuu, akaitoa roho yake. Wakati huo huo pazia la Hekalu likachanika vipande viwili, kuanzia juu hadi chini. . .Mathayo 27:50–51
Sikuona Hekalu ndani ya huo mji kwa sababu Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo ndio hekalu lake.Ufunuo 21:22
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha