Kupitia mfumo wa mji wa makimbilio katika Agano la Kale, Mungu Aliwalinda wale walioua watu bila kukusudia naye Akawaruhusu warudi katika nchi yao wenyewe kupitia tu kifo cha Kuhani mkuu. Hili linafunua kile kinachotukia katika ulimwengu wa kiroho na jinsi tunavyoweza kupokea wokovu wa Mungu.
Wanadamu wote walishuka duniani, mji wa makimbilio wa kiroho, baada ya kutenda dhambi Mbinguni, nao wanaweza kurudi katika Nchi ya Mbinguni kwa kupokea tu msamaha wa dhambi kupitia Pasaka ya agano jipya, ambayo ina damu ya thamani ya makuhani wakuu, waliopakwa mafuta matakatifu.
“Watu hawa wote walikuwa bado wanaishi kwa imani walipokufa. . . . wakikiri kwamba walikuwa wageni na wasiojulikana duniani. Watu wasemao mambo kama haya, wanaonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe. Kama wangaliifikiria nchi waliyoiacha, wangalipata nafasi ya kurudi. Badala yake, walitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni.” Waebrania 11:13–16
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha