Mungu tayari Alitabiri maafa yasiyosikiwa ambayo yanakuja katika enzi hii, kupitia manabii Wake kama vile Sefania, Malaki, Petro, na Yohana. Pia Ametuonyesha kwamba wale tu ambao wanapokea muhuri wa Mungu ambao unachukua jina jipya la Yesu—Ahnsahnghong, Mwokozi katika Enzi ya Roho Mtakatifu, waweza kuokolewa kutoka kwa maafa ya mwisho.
Katika nyakati za Agano la Kale, wale walioweka damu ya mwana-kondoo wa Pasaka kwenye nyumba zao waliokolewa kutoka kwa lile pigo. Katika enzi hii, wale tu wanaoshiriki katika mkate na divai ya Pasaka, vinavyowakilisha mwili na damu ya Yesu—uhalisia wa Mwana-kondoo wa Pasaka, waweza kupokea muhuri wa Mungu na kuokolewa kutoka maafa ya mwisho.
Waumini wa Kanisa la Mungu wanaiadhimisha Pasaka ya Agano Jipya, ambayo Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama Wamewafundisha, na kwa uaminifu wanatekeleza misheni ya kuhubiri ujumbe wa wokovu: “Pokea muhuri wa Mungu kuokolewa kutoka kwa maafa ya mwisho ambayo Mungu Ameandaa kuwahukumu waovu!”
“. . . nitawalipiza sawasawa na matendo yenu na desturi zenu za machukizo miongoni mwenu. Ndipo mtajua kuwa Mimi ndimi Bwana ambaye huwapiga kwa mapigo.” Ezekiel 7:9
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha