Kama samoni na njiwa wanavyoweza kurudi katika nchi yao ya asili haijalishi ni mbali kiasi gani, Mungu Alisema, “Nitaweka sheria yangu mioyoni mwao,” na Akaweka sheria ya agano jipya ndani ya mioyo ya wanadamu ili waweze kurudi kwenye nyumbani kwao pa milele ya mbinguni.
Miaka elfu mbili iliyopita, Yesu Alipanda mbegu nzuri [siku ya Sabato na Pasaka] kuwapa wanadamu ufalme wa mbinguni.
Walakini, zile mbegu nzuri baadaye zilitoweka na zilibadilishwa na magugu, yaani, sheria za wanadamu zilizopandwa na adui, ibilisi.
Licha ya hili, watoto wa Mungu hawalisahau kamwe agano jipya lililochorwa rohoni mwao bali wanalitambua kwa mioyo yao, na kuja kwa Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama, Wanaowaongoza kwenye ufalme wa mbinguni, nchi ya asili ya roho zao.
“Siku zinakuja,” asema BWANA, “nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda. . . .
“Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli baada ya siku zile,” asema BWANA. “Nitaweka sheria yangu katika nia zao, na kuiandika mioyoni mwao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
Yeremia 31:31–33
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha