Yule Aliyetangulia mbele ya Mfalme Koreshi na kuwashinda adui zake wote, Yule aliyeponya ukoma wa Naamani, Aliyeulinda ufalme mdogo wa Yuda dhidi ya shambulio la wanajeshi 185,000 wa Ashuru na vikosi vya washirika, na yule Aliyewapa jeshi la Yoshua ushindi katika vita dhidi ya Waamaleki ni Mungu wetu Anayeongoza kila kitu katika ulimwengu usioonekana.
Mtume Paulo alitambua kwamba hata kama mtu anapanda kiumbe hai, kukimwagilia maji, na kutengeneza mazingira ili kiweze kukua, haisaidii kitu bila Mungu Anayefanya vitu vikue.
Vivyo hivyo, waumini wa Kanisa la Mungu humtegemea Mungu ambaye yuko pamoja nao daima na huwasaidia.
Nayainua macho yangu nitazame vilima, msaada wangu utatoka wapi?
Msaada wangu hutoka kwa BWANA, Muumba wa mbingu na dunia.
Zaburi 121:1–2
BWANA asipoulinda mji, walinzi wakesha bure.
BWANA asipoulinda mji, walinzi wakesha bure.
Zaburi 127:1
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha