Gideoni alikuwa mdogo wa wote katika familia iliyokuwa kabila dhaifu zaidi miongoni mwa makabila ya Israeli. Hata hivyo aliweza kuwashinda watu 135,000 wa Midiani kwa maaskari 300 tu kwa kutii neno la Mungu. Mose na Yoshua pia walishinda vita dhidi ya Waameleki kwa kutii neno la Mungu. Kwa njia hiyohiyo, hata leo, ushindi katika hali zote huja kutokana na kuamini katika msaada wa Mungu na kumtii.
Kama tu Isaya Alivyotabiri, "Mungu Atamfanya aliye mdogo kuliko wote kuwa taifa lenye nguvu," wale wanaotambua kwamba kila kitu katika hii dunia kinatimizwa kulingana na mpango wa Mungu na kutii neno la Mungu, hata kwa kinachoonekana kidogo, kitabarikiwa.
Gideoni akauliza, “Ee Bwana wangu, . . .Ukoo wangu ndio dhaifu kuliko zote katika Manase, nami ndiye mdogo wa wote katika jamaa yangu.”
BWANA akamjibu, “Nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga Wamidiani kana kwamba walikuwa ni mtu mmoja.”
Waamuzi 6:15-16
"Ndipo watu wako wote watakuwa waadilifu, nao wataimiliki nchi milele.
Wao ni chipukizi nililolipanda, kazi ya mikono yangu, ili kuonyesha utukufu wangu. Aliye mdogo kwenu atakuwa elfu, mdogo kuliko wote atakuwa taifa lenye nguvu. Mimi ndimi BWANA; katika wakati wake nitayatimiza haya upesi.”
Isaya 60:21-22
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha