Kwa kuwa miili yetu ni hekalu la Mungu, ambalo Mungu Alinunua kwa damu Yake, hatupaswi kuwa kama Waisraeli waliojaribiwa na Shetani na kujiingiza katika uasherati mwishoni mwa safari yao jangwani na kama Esau aliyeuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa sababu ya njaa. Tunapaswa kuishi maisha ya haki ya kumfuata Mungu, na sio ulimwengu huu mwovu na wa uzinzi.
Ulimwengu unapojawa na dhambi na uzinzi, Mungu huhukumu ulimwengu. Kama vile Mungu Alivyohukumu kizazi kiovu kwa maji katika siku za Noa na kwa moto katika siku za Sodoma na Gomora, Mungu Alitabiri kupitia manabii kwmba Atahukumu kizazi hiki kiovu na cha uzinzi kwa moto na Aliwafundisha watoto Wake kuishi maisha matakatifu na ya kumcha Mungu.
Ulimwengu wa wakati ule uligharikishwa kwa hayo maji na kuangamizwa. Lakini kwa neno lilo hilo, mbingu za sasa na dunia zimewekwa akiba kwa ajili ya moto, zikihifadhiwa hadi siku ile ya hukumu na ya kuangamizwa kwa watu wasiomcha Mungu. . . . Inawapasa kuishi maisha matakatifu na ya kumcha Mungu, mkingojea na kuhimiza kuja kwa hiyo siku ya Mungu. . . . 2 Petro 3:6–12
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha