Kama vile kuna sheria katika dunia hii, Mungu pia Ana sheria kwa ajili ya wokovu wa wanadamu.
Kama Rehoboamu wa Yuda na Yeroboamu wa Israeli walivyoonyesha huko nyuma, falme na watu ambao hawafuati sheria za Mungu watapokea maafa na adhabu mwishoni.
Biblia inasema kwamba wale wanaoacha sheria ya Mungu ni wale wanaomwacha Mungu.
Miongoni mwa makanisa mengi ulimwenguni, Mungu yuko pamoja na kanisa linalozishika sheria [amri] za Mungu na kuliongoza kwenye ushindi katika maafa na hata katika vita vikuu dhidi ya Shetani.
Baada ya nafasi ya Rehoboamu kuimarika na kuwa na nguvu, yeye na Israeli yote waliiacha sheria ya BWANA Mungu.
Kwa sababu hawakuwa waaminifu kwa BWANA, Shishaki mfalme wa Misri akashambulia Yerusalemu katika mwaka wa tano wa utawala wa Mfalme Rehoboamu.
2 Mambo ya Nyakati 12:1–2
Kisha lile joka likapatwa na hasira kali kwa ajili ya huyo mwanamke na likaondoka ili kupigana vita na watoto waliosalia wa huyo mwanamke, yaani, wale wanaozitii amri za Mungu na kuushika ushuhuda wa Yesu Kristo. Lile joka likasimama kwenye mchanga wa bahari.
Ufunuo 12:17
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha