Njia ya kuepuka maafa ni kuadhimisha Pasaka ya Agano Jipya. Ni Kanisa la Mungu tu, lililoanzishwa na Kristo Ahnsahnghong Aliyekuja kwa mara ya pili kulingana na unabii wa Biblia, linaloadhimisha Pasaka ya Agano Jipya kulingana na mafundisho ya Biblia.
Mabadiliko ya tabianchi, mitetemeko ya ardhi, vimbunga, njaa, vita, na mauaji hayakomi. Kama maafa haya yatakupata, je, utaweza kuyaepuka?
Vita! Njaa! Mitetemeko ya Ardhi! Magonjwa ya Kuambukiza!
Watu waliopoteza watoto wao wanaomboleza, wakiita majina yao. Watu waliovaa nguo ya gunia na wenye njaa hula udongo na kuomboleza kwa ukimya. Sote tunatetemeka kwa hofu ya mabadiliko ya tabianchi, mitetemeko ya ardhi, vimbunga, vita, na njaa, magonjwa ya kuambukiza, ambayo yanaweza kutukumba wakati wowote.
Tafadhali sikia kilio chetu katika maafa! Ee Mungu Mwenyezi, Uliyewatoa Waisraeli kutoka kwenye maafa kwa njia ya Pasaka! Tafadhali tuhurumie na turuhusu tuijue njia ya kuokolewa kutokana na maafa haya! Tafadhali tuokoe!
Takribani miaka 3,500 iliyopita, wakati maafa makubwa ya kuwauwa wazaliwa wa kwanza yalipoletwa juu ya Misri, familia zilizoadhimisha Pasaka kwa kuwachinja wana-kondoo wenye umri wa mwaka mmoja na kuipaka hiyo damu kwenye miimo ya milango, hawakudhuriwa kwa namna yoyote.
“ ‘Damu (ya mwana-kondoo wa Pasaka) itakuwa ishara kwa ajili yenu ya kuonyesha nyumba ambazo mtakuwamo; nami nitakapoiona damu, nitapita juu yenu. Hakuna pigo la uharibifu litakalowagusa ninyi nitakapoipiga Misri . . .’ ” Kut. 12:11–14
Pasaka, yaani, ishara ya uwezo wa Mungu, inatusaidia kuepuka maafa! Pasaka iliyoadhimishwa Misri ilikuwa kivuli. Pasaka, ambayo Yesu Alianzisha kabla hajasulubiwa, ndiyo uhalisi. (Lk 22:20; Mt 26:17)
Pasaka ya Agani Jipya, ambayo kwayo tunaweza kushiriki katika damu ya thamani ya Yesu, lazima iadhimishwe katika enzi hii, pia. Walakini, kwenye Mtaguso wa Nisea uliofanyika mwaka 325 B.K., Pasaka ya Agano Jipya, ambayo kwayo damu ya thamani ya Yesu imeahidiwa, iliondolewa kabisa.
Kwa shukrani, Mungu Alisema, “Katika wakati wake nitayatimiza haya upesi” (Isa 60:22), nao wakati wake umekuja nayo Pasaka, yaani, ukweli wa Mungu, imefunuliwa, Kristo Ahnsahnghong Aliyekuja kwa mara ya pili kama ilivyotabiriwa katika Biblia Ameirudisha Pasaka ya Agano Jipya.
“Ulimwenguni kote, ni Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu tu (Mchungaji Mkuu Kim Joo-cheol) inayoadhimisha Pasaka kwa mkate na divai kama vile Karamu ya Mwisho ya Yesu Kristo.”
Ee Mungu, turuhusu tuihubiri Pasaka ya Agano Jipya, njia pekee ya kushiriki katika damu ya thamani ya Yesu, ili kwamba ulimwengu mzima uiadhimishe nao uokolewe kutokana na maafa!
Tafadhali njooni kwenye Kanisa la Mungu, lililoanzishwa na Kristo Ahnsahnghong ambaye Amekuja kwa mara ya pili kulingana na unabii wa Biblia, nanyi mwadhimishe Pasaka ya Agano Jipya, na mtaokolewa kutokana na maafa na mtapokea uzima wa milele.
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha