Mwenyezi Mungu, Aliyeumba nuru na
kuumba vitu vyote kwa neno Lake,v
Alikuja katika dunia hii kwa mara
ya pili.
Mnamo mwaka 1948 wakati matawi ya
mtini [Israeli], yaliyonyauka kwa
miaka 1,900, yalipoanza kuchipua
na kutoa majani, Kristo Alikuja
Korea, Akaanza kuhubiri injili.
Nchi, ambayo manabii wa Israeli walitabiri
kama mahali ambapo Kristo Atakuja tena,
ilikuwa pembe za mbali zaidi katika
miisho ya dunia katika Korea ya
mashariki.
Kristo Alichagua kuteseka kwa ajili ya wokovu wetu.
Walakini, tulitafuta mkate kwa ajili ya
mwili wetu, badala ya mkate wa
uzima kwa ajili ya nafsi zetu.
“Yesu Alitupa agano la uzima: ‘Ikiwa
mnaula mwili Wangu na kuinywa
damu Yangu, mnao uzima ndani yenu’.
Hakuna muujiza mkubwa zaidi kuliko huu.”
Mkate wa uzima ni mwili na damu ya Kristo.
“ ‘Twaeni mle; mkate wa Pasaka ni
mwili wangu.’ ”Mt 26:26
“ Hii [Divai ya Pasaka] ndiyo damu yangu
ya Agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi
kwa ondoleo la dhambi. ”Mt 26:27–28
Ilimbidi Kristo Aje kwa mara ya pili
na Pasaka ya Agano Jipya ili
kutuokoa.
Kabla ya Kristo kurudi Mbinguni,
Alitamani jambo moja tu:
Ni kwa ajili yenu kupokea wokovu.
Kama Kristo Asingekuja duniani,
tusingejua upendo ni nini.
Kama Kristo Asingeteseka, tusingejua dhabihu
ni nini.
Kama Kristo Angalibaki Mbinguni,
tusingalimtamani.
Tunampenda Kristo Aliyekuja kwa mara ya
pili kutuokoa.
Je, Mnasikia?
Je, unamsikia Kristo Akibisha mlango wa
moyo wako?
Kristo Anakupenda.
Anataka kukupa uzima wa milele.
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha