Mungu, ambaye Anapaswa kuketi katika kiti cha enzi kitukufu mbinguni, Alikuja hapa duniani kwa jina la Yesu miaka 2,000 iliyopita na leo kama Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama, na kwa ukimya Akaitembea njia ya dhabihu kwa ajili ya msamaha wa dhambi na wokovu wa wanadamu.
Kwa hiyo, sikuzote tunapaswa kuwa na shukrani kumwelekea Mungu Aliyetupa tumaini la mbinguni.
Wakifuata mfano wa watakatifu wa Kanisa la mapema waliotembea njia ya kifo cha kishahidi kwa shangwe licha ya mateso makali, na Mfalme Daudi ambaye sikuzote alitoa shukrani kwa Mungu licha ya magumu na majaribu, waumini wa Kanisa la Mungu wanaishi maisha ya shukrani katika hali zote.
Furahini siku zote;
ombeni bila kukoma;
shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu.
1 Wathesalonike 5:16–18
“Atoaye dhabihu za shukrani ananiheshimu mimi, naye aiandaa njia yake ili nimwonyeshe wokovu wa Mungu.”
Zaburi 50:23
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha