Mungu aliteua siku ya kuabudu kwa watu wanaomuamini yeye.
“Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.” Kut 20:8
Watu wa Mungu wanapaswa kuishika siku ya Sabato ambayo Mungu aliiteua kuwa siku ya ibada.
Mungu aliumba mbingu na dunia kwa siku sita na akapumzika katika siku ya saba, Sabato. (Mwa 2:3)
Siku ya Sabato, siku ya kuenzi nguvu ya Mungu ya uumbaji, ni siku ya saba.
Hivyo, siku gani ya wiki ni siku ya saba?
Kamusi zinasema kwamba siku ya saba ni Jumamosi.
Tunapotazama kalenda,Siku ya saba, Sabato, ni Jumamosi.
Biblia inasema kwamba Yesu alifufuka siku ya kwanza ya juma.
Kwenye mstari huo huo, Good News Bible inasema Yesu alifufuka Jumapili. (Mk 16:9)
Siku ya kwanza ya juma= Jumapili
Kwa hiyo siku gani ya wiki ni Sabato? Sabato ni Jumamosi.
Vitabu vya wakatoliki pia vinashuhudia kwamba siku ya Sabato ni Jumamosi.
“Maandiko yanasema tuitakase siku ya Jumamosi, siku ambayo hatujawahi kuitakasa.” James Cardinal Gibbons, Imani ya Baba Zetu /The Faith of Our Fathers
“Neno Sabato linamaanisha kupumzika, na ni Jumamosi, siku ya saba ya wiki.” (Rev. John A. O’Brien, Imani ya Mamilioni /The Faith of Millions
Yesu pia aliabudu siku ya Sabato [Jumamosi].
“Yesu… siku ya Sabato [Jumamosi] akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake.” Lk 4:16
Baada ya Yesu kupaa,Mtume Paulo pia aliabudu siku ya Sabato [Jumamosi]
“Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimokuwa, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko Sabato tatu…” Mdo 17:2
“Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu.Hivyo ninyi hamsikii kwa sababu ninyi si wa Mungu.” Yn 8:47
Kama ambavyo Yesu na wanafunzi wake walivyoishika siku ya Sabato [Jumamosi],
Watu wa Mungu wanapaswa kuishika siku ya Sabato [Jumamosi] iliyoteuliwa na Mungu.
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha