Kwa uweza wa Mungu, Waisraeli waliachiliwa huru kutoka utumwa wa miaka 430 huko Misri, na kuelekea Kanaani. Walakini, Waisraeli walisahau neema ya Mungu aliyewaweka huru.
“Kwa nini mmetupandisha kutoka Misri na kutuingiza katika jangwa hili?”
Watu, waliolalamika, waliumwa na nyoka wenye sumu nao wakafa (Hes 21:6).
Bwana akamwambia Mose,
“Tengeneza nyoka wa shaba na umweke juu ya mti; yeyote aliyeumwa na nyoka anaweza kumtazama na akaishi tena.” Hes 21:8
Basi, je, ni yule nyoka wa shaba aliyewaokoa?
Hapana. Mungu Aliwaokoa kwa maneno Yake, “Yeyote aliyeumwa anaweza kumtazama na kuishi.”
Hata hivyo, Waisraeli walimheshimu yule nyoka wa shaba kwa mamia ya miaka, wakifikiri kwamba alikuwa na nguvu za ajabu.
Mfalme Hezekia alipoivunja nyoka ya shaba vipande vipande, Mungu Alimpongeza, na kumfanya afanikiwe katika lolote alilofanya (2 Fal 18:3–7).
Kwa nini Mungu Alimsifu Hezekia aliyevunja nyoka ya shaba vipande vipande?
Ni kwa sababu yeye aabuduye sanamu ataharibiwa.
Historia ya kuabudu nyoka ya shaba ilikuwa unabii kwamba makanisa yatasimamisha msalaba na kuharibiwa.
Kama vile Mose alivyomwinua yule nyoka kule jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu. Yoh 3:14–15
Haikuwa msalaba uliotuokoa, bali Yesu (1 Pet 1:18–19).
Leo, walakini, makanisa yanaheshimu msalaba, kama vile Waisraeli walivyomheshimu yule nyoka wa shaba. Msalaba si kitu ila kipande cha mti, kama vile nyoka ya shaba si kitu bali kipande cha shaba (Matendo 5:30). Makanisa, yaliyosimamisha msalaba, yataharibiwa (Kumb 27:15).
“Tokeni katikati yake, enyi watu wangu, ili msije mkashiriki dhambi zake, ili msije mkapatwa na pigo lake lolote; Ufu 18:4
Likifuata mafundisho ya Kristo Ahnsahnghong Ajaye Mara ya Pili, Kanisa la Mungu linawajulisha watu wote kwamba tukio la nyoka wa shaba ni unabii wa uchaji wa msalaba.
Tafadhali njoo katika Kanisa la Mungu, ambalo ni Sayuni ambapo Mungu Mama, Mwokozi katika Enzi ya Roho Mtakatifu, hukaa, nawe utajiepusha na maafa ya mwisho na kuokolewa.
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha