Dhambi ya kula kutoka kwenye mti wa ujuzi wa mema na mabaya hupitishwa kwa wanadamu kutoka kwa Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni.
Ili wanadamu wawekwe huru mbali na dhambi, wanahitaji ukweli wa mti wa uzima unaowawezesha wale wanaoushiriki kupata uzima wa milele.
Wale tu wanaotambua dhabihu na upendo wa Kristo Ahnsahnghong na Mama wa Mbinguni, ambao Wameleta mti wa uzima, na kushika ukweli huu kwa moyo wote, wanaweza kuwekwa huru mbali na dhambi ya mauti.
Dhambi ya mauti, ambayo ilirithiwa kutoka kwa Adamu, lazima iondolewe kutoka kwa watu wanaotaka kuokolewa na kuingia katika ufalme wa mbinguni.
Kwa hiyo, Kristo Ahnsahnghong Alikuja katika dunia hii mara ya pili naye Akaleta Pasaka ya agano jipya, ukweli wa mti wa uzima, ili kuwasamehe wanadamu wote na kuwapa urithi wa ufalme wa mbinguni.
Hii ndiyo ahadi yake kwetu, yaani, uzima wa milele.
1 Yohana 2:25
Hivyo Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.
Mtu yeyote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. . . .”
Yohana 6:53–54
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha