Tunapoangalia kwa makini miujiza iliyotukia katika enzi ya Baba na katika Enzi ya Mwana kama vile jinsi Mungu Alivyogawa Bahari ya Shamu, kuufanya mji wa Yeriko uanguke, na kusimamisha jua, tunaweza kuelewa kwamba mambo yote yalifanywa kulingana na neno la Mungu.
Mungu Ahnsahnghong na Mungu Mama Walikuja katika dunia hii kama Roho na Bibi arusi katika Enzi ya Roho Mtakatifu. Kila tunapolitii neno la Mungu, tukiamini kwamba kazi ya injili inafanikishwa na Mungu, kazi ya kushangaza ya injili inatimizwa hata wakati huu.
(Manukato ya Sayuni: Kazi ya Injili iliyofanikishwa ndani ya miezi minne, baada ya tamasha la kuhubiri la Pentekoste)
Katika siku ile ambayo BWANA aliwapeana Waamori kwa Israeli, Yoshua akanena na BWANA . . . “Wewe jua, simama juu ya Gibeoni, wewe mwezi, tulia juu ya Bonde la Aiyaloni.” Hivyo jua likasimama, nao mwezi ukatulia, hadi taifa hilo lilipokwisha kujilipizia kisasi kwa adui wake, . . .
[Yoshua 10:12–13]
Ndipo Mose akanyoosha mkono wake juu ya bahari, naye BWANA akayasukuma maji ya bahari nyuma kwa upepo mkali wa mashariki usiku ule wote na kupafanya nchi kavu. Maji yakagawanyika.
[Kutoka 14:21]
Alipomaliza kunena, akamwambia Simoni, “Sasa peleka mashua hadi kilindini kisha mshushe nyavu zenu mkavue samaki.” . . . “Bwana, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha na hatukuvua chochote Lakini, kwa neno lako nitazishusha nyavu.” wakavua samaki wengi sana, nyavu zao zikajaa zikaanza kukatika.
[Luka 5:4–6]
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha