Watakatifu wa Kanisa la mapema walisali kwa dhati kwa muda wa siku kumi tangu Siku ya Kupaa hadi Siku ya Pentekoste. Siku ya Pentekoste, walipokea Roho Mtakatifu aliyewaruhusu kuwa na imani yenye ujasiri na kueneza injili kwa kasi sana. Katika Enzi ya Roho Mtakatifu, Mungu Anatujalia karama za Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste, zenye nguvu hata mara saba zaidi kuliko zile za miaka 2,000 iliyopita.
Baada ya kupokea Roho Mtakatifu, Kanisa la mapema lilishuhudia, "Yesu Ndiye Kristo." Vivyo hivyo, sasa waumini wa Kanisa la Mungu, waliopokea Roho Mtakatifu wa mvua ya mwisho kwa kuadhimisha Pentekoste, wanawahubiri kwa ujasiri Waokozi wetu, Kristo Ahnsahnghong na Mama wa Mbinguni kwa ulimwengu.
“Siku ya Pentekoste ilipowadia, waamini wote walikuwa mahali pamoja. Ghafula sauti kama mvumo mkubwa wa upepo mkali uliotoka mbinguni ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi. Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kukaa juu ya kila mmoja wao. Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia.” Matendo 2:1–4
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha