Ili kupokea msamaha wa dhambi, mtu lazima azibebe dhambi. Mungu Alituonyesha hili kama kivuli mapema kupitia wanyama waliotolewa dhabihu kwa ajili ya siku ya Sabato, sadaka ya kawaida ya kuteketezwa, Pasaka na sikukuu nyingine zote katika Agano la Kale, na pia sheria ya Agano la Kale kwamba kwenye Siku ya Upatanisho, dhambi zote ziliwekwa juu ya mbuzi wa kubebeshwa dhambi iliyopelekwa jangwani na kufa.
Waumini wa Kanisa la Mungu wanatambua kwamba Mungu Alivumilia mateso yote ya msalaba, dhihaka, na dharau ya uumbaji Wake kwa sababu ulikuwa ni upendo mkuu wa Mungu wa kutaka kuwaokoa wanadamu wote kwa kulipa gharama ya dhambi zao.
Kama tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha kutoka kwenye udhalimu wote.
1 Yohana 1:9–10
“[K]ama vile ambavyo Mwana wa Adamu hakuja ili kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai wake uwe fidia kwa ajili ya wengi.”
Mathayo 20:28
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha