Mose na Waisraeli walivumilia mateso mengi kuanzia wakati walipoadhimisha Pasaka na kuondoka Misri hadi walipovuka Bahari ya Shamu. Hii ilitimizwa na mateso ambayo Kristo Alipitia katika
Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, ambayo ilikuwa siku moja baada ya kuadhimisha Pasaka.
Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu ni sikukuu inayoonyesha kuteswa kwa Kristo, ambako ndiko uhalisi wa Sheria ya Mose katika Agano la Kale. Katika enzi hii, Mungu Alituambia tushiriki katika mateso ya Kristo kwa kufunga na kukamilishwa kwa kushinda mateso yote ambayo kila mmoja wetu atapitia.
Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu ya kwamba sisi tu watoto wa Mungu. Hivyo, ikiwa sisi ni watoto, basi tu warithi, warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo, naam, tukiteswa pamoja naye tupate pia kutukuzwa pamoja naye. Nayahesabu mateso yetu ya wakati huu kuwa si kitu kulinganisha na utukufu utakaodhihirishwa kwetu. Warumi 8:16–18
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha