Kama vile malaika Lusifa na
mfalme wa Tiro, waliokuwa
katika nafasi ya utukufu mbinguni,
walivyomsaliti Mungu kwa sababu
ya kiburi chao, wakitaka kujiinua
juu ya Mungu, wanadamu wote
walitenda dhambi mbinguni na
wakashuka chini duniani, na
walikuwa wameandikiwa tangu
zamani adhabu katika jehanamu.
Walakini, Mungu Mwenyewe
Alifanyika dhabihu ya sadaka
ya dhambi katika kila ibada na
Akatupa msamaha wa dhambi.
Kwa takribani miaka 1,500 tangu
wakati wa Mose hadi wakati wa
Yesu, Mungu Alituruhusu kupokea
msamaha wa dhambi kupitia damu
ya dhabihu ya wanyama wa kiume
na wa kike katika siku ya Sabato,
na katika kila sikukuu. Kupitia
agano la kale, Mungu Hutujulisha
dhabihu na upendo wa Mungu
Mama ambaye ni uhalisi wa agano
jipya, na Anatuonyesha dhabihu
ya Kristo Ahnsahnghong, ambaye
Alimwaga damu Yake msalabani
kama ushuhuda wa upendo Wake
kwa wanadamu.
“Mtu ambaye ni safi atakusanya
majivu ya mtamba huyo na
kuyaweka mahali ambapo ni safi nje
ya kambi kwa taratibu za kiibada.
Yatahifadhiwa na jumuiya ya
Kiisraeli kwa matumizi katika maji
ya utakaso; ni kwa ajili ya kutakasa
kutoka dhambini.”
Hesabu 19:9
“Lakini kama mtu mmoja
peke yake akitenda dhambi
pasipo kukusudia, ni lazima
alete mbuzi mke wa mwaka
mmoja kwa ajili ya sadaka ya
dhambi.”
Hesabu 15:27
Hili ndilo asemalo BWANA: “Iko
wapi hati ya talaka ya mama yako
ambayo kwayo niliachana naye?
Au nimewauza ninyi kwa nani
miongoni mwa watu wanaonidai?
Kwa ajili ya dhambi zenu mliuzwa,
kwa sababu ya makosa, mama
yenu aliachwa.”
Isaya 50:1
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha