Mungu Aliwaruhusu Waisraeli wapige
tarumbeta ya toba katika Sikukuu ya Tarumbeta,
siku ya kwanza ya mwezi wa saba kulingana na
kalenda takatifu ili kujiandaa kwa ajili ya
Siku ya Upatanisho, siku ya kumi ya mwezi wa
saba kulingana na kalenda takatifu wakati Mose
alipokea zile Amri Kumi kwa mara ya pili.
Kiroho, ni sikukuu inayowahimiza
wanadamu wote, ambao wametenda
dhambi zisizosameheka mbinguni na
wakafukuzwa hadi kwenye dunia hii,
kutubu, kwa kusema, “Tubuni kupitia
agano jipya na mrudieni Mungu.”
Leo, ufalme wa mbinguni unapokaribia,
wale walioahidiwa ufalme wa mbinguni
kupitia toba kamili lazima wapige tarumbeta
kuhusu dhabihu na upendo wa Mungu
Aliyewaokoa kupitia agano jipya ili kwamba
ulimwengu wote uweze kutubu na kumrudia
Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama.
“Waambie Waisraeli: ‘Katika siku ya
kwanza ya mwezi wa saba mtakuwa na
siku ya mapumziko, kusanyiko takatifu
la ukumbusho litakaloadhimishwa
kwa kupiga tarumbeta.”
Walawi 23:24
akisema, “Wakati umewadia, Ufalme
wa Mungu umekaribia. Tubuni na
kuiamini Habari Njema.”
Marko 1:15
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha