Mambo yanayompendeza Mungu
yameandikwa katika vitabu vya Luka,
Waebrania, Yeremia, na Mithali. Ni toba
ya mwenye dhambi, imani ya
kweli, kujisifu juu ya Mungu, na wale
ambao njia zao hazina lawama.
Mungu Alitufundisha kwamba haya
yote yanaweza kutimizwa kupitia kazi
ya kuhubiri inayoongoza watu wengi
kwenye wokovu.
Watoto katika dunia hii huwapa
wazazi wao zawadi zinazowapendeza
wazazi wao kwa mioyo yao yote. Vivyo
hivyo, watoto wa mbinguni hufanya yale
yanayompendeza Baba wa Mbinguni
Kristo Ahnsahnghong na Mungu
Mama zaidi. Kama vile Yesu
Alivyoamuru miaka 2,000 iliyopita,
wao hujitolea mioyo yao kutafuta
wanafamilia wa mbinguni waliopotea.
Kwa maana zamani ninyi mlikuwa
giza, lakini sasa ninyi ni nuru katika
Bwana. Enendeni kama watoto wa
nuru (kwa kuwa tunda la nuru
hupatikana katika wema wote, haki
na kweli), nanyi tafuteni yale
yanayompendeza Bwana.
Waefeso 5:8–10
[A]nayetaka watu wote waokolewe
na wafikie kuijua kweli.
1 Timotheo 2:4
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha