Vile vibao vya mawe vya kwanza vya Amri Kumi vilivunjwa vipande vipande kwa kuwa Waisraeli waliabudu ndama ya dhahabu. Walakini, Mungu Alitoa vibao vya mawe vya pili vya Amri Kumi siku ya kumi ya mwezi wa saba kwa watu waliotubu. Mungu Aliamuru siku hii kuwa Siku ya Upatanisho ambayo ina ahadi ya msamaha wa dhambi, naye Akaamuru siku ya kwanza ya mwezi wa saba kuwa Sikukuu ya Tarumbeta.
Mtume Yohana alisema kwamba sala zote zinakuwa moshi wa uvumba nazo zinapanda juu mbele za Mungu.
Lazima tutambue kwamba Roho Mtakatifu Ahnsahnghong na Mungu Mama Wanawaombea wanadamu ambao ni wadhaifu, hufuatilia mambo yasiyo na maana, nao hushindwa kuona baraka za milele Mbinguni. Ni lazima tuadhimishe Sikukuu za Mungu kwa moyo wa toba, tukitoa shukrani kwa ajili ya neema Yao.
'Lakini tunapotumaini kupata kitu ambacho hatuna, basi twakingojea kwa saburi. Vivyo hivyo, Roho hutusaidia katika udhaifu wetu, kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo. Lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa uchungu usioweza kutamkwa.' Warumi 8:25–26
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha