Amri Kumi za kwanza alizopokea Mose zilivunjwa kwa sababu Waisraeli waliabudu ndama ya dhahabu.
Baada ya Waisraeli kutambua dhambi zao na kutubu, Mose alishuka chini akiwa na seti ya pili ya Amri Kumi ambayo Mungu Aliwajalia kama ishara ya msamaha.
Hii ikawa chimbuko la Siku ya Upatanisho.
Mtu anapotenda dhambi, dhambi hiyo inahamishiwa kwa Mungu, yaani, patakatifu, kwa muda hadi Siku ya Upatanisho.
Baada ya kuhani mkuu kuingia Patakatifu pa Patakatifu na kufanya sherehe ya kunyunyiza damu, dhambi hiyo inasamehewa kabisa.
Vivyo hivyo, leo, bila kupokea neema ya Yerusalemu, ambaye ni Patakatifu pa Patakatifu, yaani, Mungu Mama, hakuna awezaye kupata msamaha kamili wa dhambi wala wokovu.
“Aroni atakapokuwa amemaliza kufanya upatanisho kwa ajili ya Patakatifu pa Patakatifu, Hema la Kukutania na madhabahu, atamleta mbele yule mbuzi aliye hai.
Aroni ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha mbuzi aliye hai na kuungama juu yake uovu wote na uasi wa Waisraeli, yaani dhambi zao zote, ili kuziweka juu ya kichwa cha huyo mbuzi. Atamwachia huyo mbuzi akimbilie jangwani kwa uangalizi wa mtu aliyepewa wajibu huo.
Yule mbuzi atachukua juu yake dhambi zao zote mpaka mahali pasipo na watu; naye yule mtu atamwachia akimbilie jangwani.”
Mambo ya Walawi 16:20–22
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha