Wanafunzi, walioshuhudia kupaa kwa Yesu kutoka Mlima wa Mizeituni, walitambua kwamba bila kuvikwa na Roho Mtakatifu wa Mungu, injili isingeweza kuhubiriwa duniani kote.
Hivyo, waliomba kwa dhati kwa muda wa siku kumi kuanzia Siku ya Kupaa hadi Siku ya Pentekoste, wakiomba Roho Mtakatifu wa mvua ya kwanza.
Eliya alipowashinda manabii 850 wa uongo kwenye Mlima Karmeli, sala ilitangulia ushindi.
Yesu, Kristo Ahnsahnghong, na Mungu Mama, Waliokuja hapa duniani kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, Waliweka kielelezo kwa kuanza kazi Yao ya injili kwa sala za mapema kila siku.
Kwa hiyo, waumini wa Kanisa la Mungu, pia, wanaanza siku yao, wakipata nguvu za kiroho kupitia sala.
“Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni nanyi mtafunguliwa mlango.
Kwa kuwa kila aombaye hupewa; naye kila atafutaye hupata; na kila abishaye hufunguliwa mlango.
Mathayo 7:7–8
Kwa sababu hiyo nawaambia, yoyote mtakayoyaomba mkisali, aminini ya kwamba mmeyapokea, nayo yatakuwa yenu.
Marko 11:24
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha