Kama vile Mungu Alivyokuwa na kusudi kubwa la kuwabariki Waisraeli hatimaye baada ya miaka yao 40 jangwani, leo, Mungu Anaweza kuweka magumu na vikwazo kwenye njia yetu ya imani, lakini kusudi Lake kuu ni kuzikamilisha roho zetu na kutupatia baraka za ufalme wa mbinguni.
Dunia ni gereza la kiroho ambapo malaika wa mbinguni waliokuwa wametenda dhambi nzito walitupwa chini ili waishi. Ndiyo maana katika dunia hii, nyakati za maumivu na mateso hutokea mara nyingi zaidi kuliko zile za amani na furaha. Ili kufuta dhambi hizi za wanadamu, Mungu Alimwaga damu Yake msalabani na akatufungulia njia ya kurudi katika ufalme wa mbinguni kupitia Pasaka ya agano jipya, njia ya msamaha wa dhambi.
Aliwapa mana ya kula jangwani, kitu ambacho baba zenu hawakukijua, ili kuwanyenyekeza na kuwajaribu ninyi, na mwishoni apate kuwatendea mema. Kumbukumbu la Torati 8:16
Kwa maana Mwana wa Adamu amekuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea.” Luka 19:10
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha