Aleksander Mashuhuri, ambaye alishinda robo ya ulimwengu, na kutukuzwa sana na watu,
naye pia alimaliza maisha yake kwa ubatili.
Ijapokuwa mtu anamiliki kila kitu ulimwenguni, kama yeye hajui kuhusu ulimwengu wa milele,
maisha yake ni ubatili mtupu. Ijapokuwa alikuwa na kila kitu chenye thamani ya vitu vya anasa— nguvu, utajiri, heshima, hakuweza kujiandaa kwa ulimwengu wa milele na hatimaye akafa!
Utajiri, heshima na nguvu za ulimwengu huu hazidumu kwa muda mrefu,
bali hazina maana mbele ya kifo.
Hivyo Kristo Ahnsahnghong Alituambia tujiandae kwa ulimwengu wa kiroho ambako kuna shangwe ya milele. Ni kwa sababu kiini chetu sio miili yetu bali nafsi zetu. (Yohana 6:63)
Maisha bila kujua kuhusu ulimwengu wa kiroho ni ubatili mtupu.
Maisha yetu mafupi katika dunia hii ni muda wa kujiandaa kwa ulimwengu wa kiroho.
Je, tunapaswa kufanya nini ili kwenda kwenye ulimwengu wa milele wa kiroho?
Ulimwengu wa milele wa kiroho bila maumivu wala mauti, (Ufunuo 21:4) mwili uharibikao hauwezi kuingia, bali yeye tu ambaye ana uzima wa milele anaweza kuuingia. (1 Wakorintho 15:50)
Basi, tunawezaje kuwa na uzima wa milele?
Tunapokula mwili wa Yesu na kunywa damu Yake, tunaweza kuwa na uzima wa milele. (Yohana 6:54)
Yesu Aliahidi kwamba mkate na divai ya Pasaka ni mwili na damu Yake. (Mathayo 26:26)
Hivyo wale wapatao uzima wa milele kwa njia ya Pasaka wanaweza kuingia katika ulimwengu wa kiroho, ambako watasafiri kwa uhuru katika ulimwengu wa juu. Hebu tuutazamie ulimwengu wa milele wa kiroho, badala ya kupoteza maisha yetu bure, tukizingatia tu juu ya ulimwengu wa vitu vya anasa, na hebu tushiriki katika ahadi takatifu ya uzima wa milele [Pasaka].
Kanisa la Mungu Alilolianzisha Kristo Ajaye Mara ya Pili Ahnsahnghong ni kanisa pekee linalofuata Agano Jipya ya Pasaka.
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha