Sikukuu ya Malimbuko iliyoadhimishwa wakati wa Mose
katika Agano la Kale ilikuwa ni kivuli, na
Siku ya Ufufuo ya Agano Jipya ndio uhalisi.
Yesu Kristo Alifufuka mapema asubuhi
kwenye siku baada ya siku ya Sabato, Jumapili,
kama malimbuko ya wale waliolala
kuutimiza unabii wa Sikukuu ya Malimbuko.
Kwa hiyo, ni mapenzi ya Mungu kwamba tunaishika
Siku ya Sabato (Jumamosi) kama sikukuu ya kila wiki,
na Siku ya Ufufuo kama sikukuu ya kila mwaka.
Shetani aliwaweka wanadamu chini ya mnyororo wa mauti,
akiwafanya wapitie uchungu wa mauti;
walakini, Yesu Kristo Alikuja katika dunia hii,
Akivunja nguvu ya mauti, na kuongoza watu
kwenye ukweli unaoelekea uzima wa milele
kupitia Siku ya Ufufuo.
Siku hizi, waumini wa Kanisa la Mungu
hawafuati tamaduni ya kipagani ya kushiriki mayai,
bali wanamega mkate unaoyafumbua macho yetu ya kiroho,
wakifuata kielelezo cha Yesu Kristo.
“Lakini kweli Kristo amefufuliwa kutoka kwa wafu,
tunda la kwanza la wale wote waliolala . . .
katika Kristo wote watafanywa hai.” [1 Wakorintho 15:20–22]
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha