Matendo ya kila mtu, yaliyoandikwa katika Kitabu cha Uzima, hayafutwi hata baada ya maelfu ya miaka, ila yatahukumiwa na Mungu kama yanastahili thawabu au adhabu. Kwa sababu hiyo, watashiriki katika ufufuo wa wenye haki, ambao utawaongoza kuelekea Mbinguni, au ufufuo wa wasio na haki ambao utawaongoza kuelekea jehanamu.
Watakatifu wa Kanisa la mapema walipata kujionea ufufuo wa Yesu na kusimama imara katika imani yao. Leo, Kristo Ahnsahnghong na Mama wa Mbinguni Wanatufundisha kuwa na imani katika kufufuliwa na kubadilishwa. Wanatufundisha kwamba wanadamu wote wanapomwogopa Mungu na kutubu dhambi zao kabisa, watabadilishwa na kuwa na miili ya kiroho na kurudi katika ulimwengu wa malaika.
“[N]ami ninalo tumaini kwa Mungu, ambalo hata wao wenyewe wanalikubali kwamba kutakuwa na ufufuo wa wenye haki na wasio na haki. Kwa hiyo ninajitahidi siku zote kuwa na dhamiri safi mbele za Mungu na mbele za wanadamu.”
Matendo 24:15–16
Lakini uenyeji wetu uko mbinguni. Nasi tunamgoja kwa shauku Mwokozi kutoka huko, yaani, Bwana Yesu Kristo, . . . atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, ili upate kufanana na mwili wake wa utukufu.
Wafilipi 3:20–21
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha