Tunapokumbwa na majaribu, taabu, na mizigo mizito ya msalaba katika njia yetu ya imani, wale wanaoona magumu haya kama mateso, wakifikiri, “Nina bahati mbaya,” hakika watakuwa wasio na furaha, lakini wale wanaotambua baraka na kutoa shukrani katika hali hizi watapata furaha na kuingia Ufalme wa Mbinguni.
Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama Wanasema, “Furahini siku zote shukuruni kwa kila jambo,” na kutufundisha tuishi maisha ya kutosheka kwa sababu ulafi wa ulimwengu hutengeneza majaribu na huzuni. Wanatufundisha tuweke katika utendaji kujizoeza wenyewe kuwa watauwa kwa kubadili kila hali ya bahati mbaya kuwa nguvu yenye furaha.
Furahini siku zote; ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo,
kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu.
1 Thesalonike 5:16–18
Heri mtu anayevumilia wakati wa majaribu, kwa sababu akiisha kushinda hilo jaribio atapewa taji la uzima Mungu alilowaahidia wale wampendao. . . . Lakini kila mtu hujaribiwa wakati anapovutwa na kudanganywa na tamaa zake mwenyewe zilizo mbaya. Basi ile tamaa mbaya ikishachukua mimba, huzaa dhambi, nayo ile dhambi ikikomaa, huzaa mauti.
Yakobo 1:12–15
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha