Siku ya Malimbuko katika Agano la Kale ni Siku ya Ufufuo katika Agano Jipya. Ni unabii ambao ulitakiwa utimie siku ya Jumapili.
Ilikuwa siku ya kwanza ya juma Waisraeli walipotoka Misri na kuvuka ng’ambo ya Bahari ya Shamu. Mungu Aliiamuru siku hii kuwa Siku ya Malimbuko, na kuwaamuru Waisraeli waiadhimishe siku inayofuata Sabato (Jumapili) kila mwaka. Yesu Alifufufka siku ya kwanza ya juma (Jumapili), Akiutimiza unabii wa Siku ya Malimbuko.
Kulingana na unabii wa Siku ya Malimbuko, mganda wa nafaka ya kwanza ulipotolewa kwa Mungu, Yesu Alifufuka kama limbuko la wale waliolala na Akawapa wanadamu wote tumaini la ufufuo. Likiamini haya, Kanisa la Mungu linaadhimisha Siku ya Ufufuo kila mwaka.
BWANA akamwambia Mose, “. . . leteni kwa kuhani mganda wa nafaka ya kwanza mtakayovuna.
Naye atauinua huo mganda mbele za BWANA ili ukubaliwe kwa niaba yenu; kuhani ataupunga siku inayofuata Sabato.”
Walawi 23:9–11
Mnamo siku ya kwanza ya juma, alfajiri na mapema, wale wanawake walichukua yale manukato waliyokuwa wameyaandaa, wakaenda kaburini. Wakakuta lile jiwe limevingirishwa kutoka kwenye kaburi, lakini walipoingia ndani, hawakuuona mwili wa Bwana Yesu. . . . “Kwa nini mnamtafuta aliye hai miongoni mwa wafu? Hayuko hapa; amefufuka!”
Luka 24:1–6
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha