Yesu Alisema kwamba maji ya uzima
yanayotolewa kwenye Sikukuu ya Vibanda
ni Roho Mtakatifu wa mvua ya mwisho.
Nabii Zekaria, Ezekieli na Mtume Yohana
walishuhudia kwamba Mama wa Mbinguni
Yerusalemu, ambaye Anaitwa Kiti cha Enzi
cha Mungu, ndiye Chanzo cha maji ya
uzima. Na walishuhudia kwamba Atawapa
wanadamu uzima wa milele katika
enzi hii ya Roho Mtakatifu.
Kanisa la Mungu linaamini katika maneno
haya, “Yeyote anayemjua Mungu
atapokea Roho Mtakatifu wa mvua
ya mwisho.”
Wanatekeleza misheni kama walinzi
kuwatangazia wanadamu wote kwa usahihi
kwamba lazima waje kupokea wokovu
kutoka kwa Kristo Ahnsahnghong na
Mungu Mama, na pia kupokea Roho
Mtakatifu wa mvua ya mwisho kwenye
Sikukuu ya Vibanda.
Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa
imekaribia. . . . Yesu akiwa amesimama
huko, akapaza sauti yake akasema,
“Kama mtu yeyote anaona kiu na aje
kwangu anywe.Yeyote aniaminiye mimi,
kama Maandiko yasemavyo, vijito vya
maji ya uzima vitatiririka ndani mwake.”
Yesu aliposema haya alimaanisha
Roho Mtakatifu ambaye wote
waliomwamini wangempokea,
Yohana 7:2–39
Roho na bibi arusi wanasema, “Njoo!”
Naye asikiaye na aseme, “Njoo!”
Yeyote mwenye kiu na aje,
na kila anayetaka na anywe
maji ya uzima bure.
Ufunuo 22:17
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha