Eliya peke yake alipigana dhidi ya manabii wa uongo 850; mvulana Daudi alimshinda jitu Goliathi; Mashujaa 300 wa Gideoni walipigana dhidi ya jeshi la Wamidiani 135,000; Waisraeli waliteseka jangwani kwa miaka 40, na watakatifu wa Kanisa la mapema walihubiri injili wakiwa wanakabili mateso na kifo cha kishahidi. Katikati ya taabu, mioyo yao ilisafishwa, na imani yao ilikubaliwa na Mungu; mwishowe, walipokea utukufu wa ushindi.
Mungu Alitangulia kuona kwamba watoto Wake wangeteseka na kuzuiliwa na ibilisi. Ila, kwa njia ya usafishaji, kwanza Aliwaongoza kusitawisha uchaji Kwake, pamoja na imani, tumaini, upendo, na roho inayokataa uovu na kufuata mema, kabla ya kuwatendea miujiza kwa uweza Wake mkuu.
Kalibu husafisha fedha na tanuru husafisha dhahabu, bali BWANA huujaribu moyo. Mithali 17:3
‘‘Ni mimi nitangazaye mwisho tangu mwanzo, naam, tangu zamani za kale, mambo ambayo hayajatendeka. Ninasema: Kusudi langu ndilo litakalosimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.’’ Isaya 46:10
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha