Hata leo, katika amri ya Mungu ya kushika agano jipya kama vile siku ya Sabato na Pasaka, kuna mapenzi Yake ya kina kama vile Mungu Alipowaambia Adamu na Hawa katika Bustani ya Edeni,
“Msile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya” ili kuwabariki.
Ina dhamira kuu ya kuwatakia wanadamu baraka kupitia agano jipya.
Tukitegemea tu uzoefu na maarifa yetu wenyewe na kuyahesabu maneno ya Mungu kuwa duni, mwishowe taabu na maafa yatatufuata.
Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama Wametufundisha kwamba tunapoona neno la Mungu kuwa la thamani kama Danieli, Shadraki, Meshaki, na Abednego walivyolifanya, tutapokea baraka na utukufu ambao utashangaza ulimwengu.
Uwe mwangalifu kufuata kila agizo ninalokupa wewe leo, ili mweze kuishi, kuongezeka na mweze kuingia mkamiliki nchi ambayo BWANA aliahidi kwa kiapo kwa baba zenu.
Kumbukumbu la Torati 8:1
Kama ukimtii BWANA Mungu wako kwa bidii na kufuata amri zake zote ninazokupa leo kwa bidii, BWANA Mungu wako atakuweka juu ya mataifa yote katika dunia.
Kumbukumbu 28:1
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha