Mchungaji ni muhimu zaidi kuliko mfalme kwa kondoo aliyepotea, na maji ni ya thamani zaidi kuliko dhahabu jangwani.
Thamani ya amri za Mungu itadhihirishwa wanadamu watakaposimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu.
Hii ni kwa sababu mbingu na jehanamu huamuliwa kulingana na kama mtu amezishika amri za Mungu au la.
Kwa kuwa ufalme wa mbinguni ni mahali ambapo wenye dhambi hawawezi kuingia, ni lazima wapokee msamaha wa dhambi zao.
Mungu Ameahidi msamaha wa dhambi katika damu ya thamani ya Kristo kupitia Pasaka ya agano jipya.
Kwa hiyo, kama Daudi, wanadamu lazima wawe na imani katika ahadi ya Mungu na wazipende amri Zake.
Kwa sababu nazipenda amri zako zaidi ya dhahabu, naam, zaidi ya dhahabu safi, . . .
Zaburi 119:127
“ ‘Mwalimu asema hivi: Saa yangu imekaribia. Nitaiadhimisha Pasaka pamoja na wanafunzi wangu katika nyumba yako.’ ”
Hivyo wanafunzi wakafanya kama vile Yesu alivyokuwa amewaelekeza, nao wakaandaa Pasaka.
. . . “Nyweni nyote katika kikombe hiki. Hii ndiyo damu yangu ya Agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.”
Mathayo 26:18–28
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha