Kama vile Adamu na Eva walivyopoteza utukufu wa Bustani ya Edeni kwa sababu ya dhambi ya kula kutoka kwenye mti wa kujua mema na mabaya, wanadamu walipoteza utukufu wote kwa sababu ya dhambi zao mbinguni nao wakatupwa chini duniani. Wanadamu walitenganishwa na Mungu kwa sababu ya dhambi zao, lakini Mungu Amewaruhusu kumwabudu Yeye kupitia sikukuu saba katika nyakati tatu, ikiwemo siku ya Sabato na Pasaka, kama njia ya kuwasamehe dhambi zao.
Tunaweza kuthibitisha katika Biblia kwamba dhabihu ya Abeli, iliyompendeza Mungu, iliwakilisha kwamba Kristo Atazisamehe dhambi za wanadamu kwa kumwaga damu Yake msalabani. Kupitia dhabihu ya damu, yaani, ibada, wanadamu wanaweza kumkaribia Mungu na kuwa sehemu ya familia ya Mungu kama wana na binti za Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama, Waokozi katika nyakati za Roho Mtakatifu.
Lakini sasa katika Kristo Yesu, ninyi ambao hapo kwanza mlikuwa mbali na Mungu, sasa mmeletwa karibu kwa njia ya damu ya Kristo. . . Hivyo basi, ninyi sasa si wageni tena wala wapitaji, bali mmekuwa wenyeji pamoja na watakatifu na pia jamaa wa nyumbani mwake Mungu. Waefeso 2:13, 19
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha