Mungu, Mwokozi wa wanadamu, Ametujalia baraka za msamaha wa dhambi na ufalme wa milele wa mbinguni kwa njia ya Pasaka na kutangaza kwa nguvu kwamba wale wanaoadhimisha Pasaka watatambuliwa kuwa watu wa Mungu ambao watapokea uraia wa mbinguni na kupata wokovu.
Yesu Aliyekuja miaka 2,000 iliyopita vilevile na Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama katika enzi hii kwa mfululizo Walitufundisha kwamba kumwita Mungu kwa midomo yetu tu bila kuiadhimisha Pasaka ni sawa na imani isiyo wazi.
Pia, sababu ya Mungu kutoa Pasaka ya Pili kwa wale ambao hawakuweza kuiadhimisha wakati ulioamriwa ni kwa sababu Pasaka ni sikukuu muhimu sana inayotofautisha watu wa kweli wa Mungu.
“Waamuru Waisraeli waadhimishe Pasaka katika wakati ulioamriwa. . . .
Lakini baadhi yao hawakuweza kuadhimisha Pasaka siku ile kwa sababu walikuwa najisi kwa taratibu za kiibada kwa ajili ya kugusa maiti. . . .
Ndipo BWANA akamwambia Mose,
. . . hata hivyo wanaweza kuadhimisha Pasaka ya BWANA.
Wataiadhimisha wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili. . . .
Lakini kama mtu . . .
asipoadhimisha Pasaka, mtu huyo hana budi kukatiliwa mbali na watu . . .”
Hesabu 9:2–13
Hivyo, mtawatambua kwa matunda yao.
“Si kila mtu aniambiaye, ‘Bwana, Bwana,’ atakayeingia katika Ufalme wa Mbinguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
Mathayo 7:20–21
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha