Yesu Mwenyewe Aliweka kielelezo cha kuwaokoa wanadamu kutoka dhambini kwa njia ya kuhubiri. Alitupa misheni ya kuwa mfanyakazi wa agano jipya, Akisema, “Okoa ulimwengu.” Kwa hiyo, lazima tusiwe kama Esau, ambaye alifanya tu kile alichotaka, bali tuwe kama Yakobo, ambaye kwanza alifanya yale aliyopaswa kufanya. Ndipo tu tutakapoweza kupokea baraka ambazo Mungu hutoa.
Matokeo ya wale wanaofanya yawapasayo kuyafanya dhidi ya wale wasiofanya ni tofauti kati ya ufalme wa mbinguni na jehanamu. Kama vile kazi ya kushangaza ya Roho Mtakatifu sikuzote ilivyokuwa pamoja na mitume walioishi maisha ya kuhubiri kama Yesu, wajibu wetu sasa ni kutangaza wokovu wa Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama.
Ndiye alitutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya: si wa andiko, bali wa Roho; kwa kuwa andiko huua, bali Roho hutia uzima. 2 Wakorintho 3:6
Yesu akawajibu, “Twendeni mahali pengine, kwenye vijiji jirani, ili niweze kuhubiri huko pia. Maana nilikuja kwa kusudi hili.” Marko 1:38
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha