Kuifuata njia ya Kristo kwa usahihi, lazima tuuchukue msalaba wetu wenyewe. Yesu, ambaye ni Mungu, Alibeba mzigo wa msalaba kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, na baba wa imani kama Mose na Mtume Paulo walichukua msalaba wao wa mateso kwa shangwe. Vivyo hivyo, sisi pia lazima tuubebe msalaba wetu wenyewe na tutembee njia ya mateso kwa ajili ya wokovu.
Kama vile Mtume Paulo alivyoona mateso yote kama baraka, akiifuata njia ya msalaba wa Kristo, waumini wa Kanisa la Mungu huchukua msalaba wao kwa furaha wakati wowote na kufuata njia ya Mungu kwa imani thabiti, bila kusahau kutoa shukrani kwa Mungu.
Heri wanaoteswa kwa sababu ya haki, maana Ufalme wa Mbinguni ni wao. “Heri ninyi watu watakapowashutumu, na kuwatesa na kunena dhidi yenu mabaya ya aina zote kwa uongo kwa ajili yangu. Furahini na kushangilia kwa maana thawabu yenu ni kubwa mbinguni, kwa kuwa hivyo ndivyo walivyowatesa manabii waliokuwa kabla yenu.” Mathayo 5:10–12
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha