Esau na Yuda Iskariote walipoteza baraka kwa sababu ya maneno ya kutojali waliyozungumza, na mnyang'anyi kwenye wa upande wa kulia na marafiki watatu wa Danieli walipokea baraka zinazofurika kutoka kwa Mungu kwa sababu ya maneno waliyozungumza kwa imani.
Kwa kuwa maneno ambayo yametoka vinywani mwetu hayatoweki kamwe bali yanaturudia katika Siku ya Hukumu, Mungu hutufundisha daima tufikiri mara nyingi kabla ya kunena na tusiwe wepesi wa kukasirika.
Tukitambua kwamba tulitupwa kutoka mbinguni kwa sababu tulitenda dhambi, hatutasikitishwa na chochote. Badala yake, tunaweza kuishi maisha yenye baraka kwa kushukuru na kusema mambo mema tukifuata mafundisho ya Mungu kwa ukweli kwamba tunaweza kuwa pamoja na Kristo Ahnsahnghong na Mungu Mama ambao Wamekuja katika enzi ya Roho Mtakatifu.
Ndugu zangu wapendwa, fahamuni jambo hili: Kila mtu awe mwepesi wa kusikiliza, lakini asiwe mwepesi wa kusema wala wa kukasirika. Kwa maana hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu. . . . Basi kuweni watendaji wa Neno wala msiwe wasikiaji tu, huku mkijidanganya nafsi zenu. . . . atabarikiwa katika kile anachofanya.
Yakobo 1:19–25
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha