Kama ambavyo uzi wa timazi unawekwa kuona kama jengo linajengwa wima au la, Mungu Anawapa watoto Wake majaribu ili kuona kama wanaijenga nyumba ya imani wima kama vile Mungu Alivyowafanyia Ayubu, Shedraki, Meshaki, na Abednego. Walakini, sikuzote baraka hufuata mwishowe.
Kristo Ahnsahnhong na Mungu Mama Wamewafundisha waumini ambao wanajenga nyumba zao za imani leo kwamba Mungu Anapoujaribu ulimwengu wote, Atachunguza maneno, matendo, na mioyo ya kila mmoja kisha Ataleta maafa juu ya wasio waaminifu ambao hunung’unika na hulalamika. Pia Wamewafundisha waumini kufikiria sikuzote kuhusu Mbinguni na Mungu tu hali iwayo yote.
Hili ndilo alilonionyesha katika maono: Bwana alikuwa amesimama karibu na ukuta ambao ulikuwa umejengwa kwa timazi, akiwa na uzi wa timazi mkononi mwake. . . . Kisha Bwana akasema, “Tazama, ninaweka uzi wa timazi miongoni mwa watu wangu Israeli; sitawahurumia tena.”
Amosi 7:7–8
“Nami nitawaua watoto wake. Nayo makanisa yote yatajua kwamba Mimi ndiye nichunguzaye mioyo na nia, na kwamba nitamlipa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.”
Ufunuo 2:23
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha