Mtume Paulo alikuwa nabii mkuu kwa sababu alikuwa ameushuhudia utukufu wa mbingu ya tatu. Ndani ya ulimwengu mpana ambao mwanadamu hawezi kuufahamu, Mungu Ametuandalia mustakabali mtukufu. Hii ndiyo sababu Ametuita tuwe na mtazamo mpana zaidi, tusiitazame dunia, bali ulimwengu—yaani, ufalme wa mbinguni.
Ni lazima tuyashinde magumu ya leo kwa kuzingatia utukufu wa ufalme wa mbinguni na mustakabali mzuri unaotungoja huko. Tukishindwa kuamini katika ufalme wa mbinguni, hatimaye tutapoteza imani yetu katikati ya mateso ya muda na kuuacha ukweli. Hata hivyo, tukiufahamu uhalisi wa ufalme wa mbinguni, imani yetu itakua siku baada ya siku, ikituwezesha kushiriki katika utukufu wake.
Kwa maana kuwa na nia ya mwili ni mauti, bali kuwa na nia inayoongozwa na Roho ni uzima na amani. Warumi 8:6
Kwa kuwa tuliokolewa kwa tumaini hili. Lakini kama kinachotumainiwa kikionekana, basi hakiwi tumaini tena. Je, kuna mtu anayetumaini kupata kitu alicho nacho tayari? Lakini tunapotumaini kupata kitu ambacho hatuna, basi twakingojea kwa saburi. Warumi 8:24–25
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha