Wanadamu wote walikuwa wenye dhambi nzito ambao walistahili adhabu ya Mungu kwa ajili ya dhambi zilizotendwa mbinguni, lakini Mungu Alikuja katika dunia hii katika mwili naye Akatujalia msamaha wa dhambi kupitia agano jipya ili kwamba tuweze kutumainia ufalme wa mbinguni tena kama watoto wa Mungu.
Mungu Alikuja katika dunia hii, ambapo Alipatwa na maumivu ya msalaba, kwa mara nyingine tena kulirudisha agano jipya ambalo lilikuwa limepotea wakati wa Enzi za Giza na kufungua njia ya wokovu kwa ajili ya wanadamu. Watoto wa Mbinguni walipokea upendo wa Mungu, ambao hata maumivu ya kifo hayakuweza kuzuia. Hivyo, kaka na dada katika Sayuni, ambao walikuja kuwa familia ya mbinguni, wanapaswa kuweka katika vitendo upendo walioupokea kutoka kwa Mungu kwa kupendana.
“Amri mpya nawapa: Mpendane kama mimi nilivyowapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi mpendane. Yohana 13:34
119 Bundang S.L.P, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jam. ya KOREA
Simu 031-738-5999 Faksi 031738-5998
Makao Makuu: 50, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Kanisa Kuu: 35, Sunae-ro, Bundang-gu, Seongnam-si, Gyeonggi-do, Jamhuri ya Korea
Jamii ya Misheni ya Dunia ya Kanisa la Mungu. Haki zote zimehifadhiwa. Sera ya Faragha